Na Shani Mhando, Morogoro

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jinsia katika Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Wazee na Watoto Bi.Mboni amefurahishwa kuanzishwa   kwa mtandao wa wanawake katika jeshi a magereza nchini

akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya  mtandao huo, uliofanyika katika ukumbi wa Umwema Mkoani Morogoro,Bi Mboni amesema, hii ni hatua nzuri sana yakupongezwa kwa Jeshi la Magereza kuhakikisha wanawake  katika Nyanja zote wanatumia fursa mbalimbali zilizopo na zitakazojitokeza ndani ya Jeshi na Nje ya Jeshi ili kujipatia mafanikio.

aliongeza kuwa msingi wa kuwepo kwa mitandao ya wanawake ni nchini ni kuwawezesha na kuwajengea uwezo  wanawake katika Nyanja za kiuchumi,mafunzo,ajira,uongozi na maamuzi ili kuweza kutimiza majukumu yao bila kubaguliwa jinsia zao.

“Ni matarajio yangu kuwa kuanzishwa kwa mtandao huu Jeshi la magereza litazingatia miongozo na kanuni mbalimbali zilizotolewa na serikali kuhakikisha katika maeneo yote yenye changamoto za usawa wa kijinsia mwanamke awezeshwe ili aweze kukabilina nazo,”alisema Bi Monica

Aidha Bi Mboni amewaasa washiriki wa mafunzo kuzingatia yote watakayofundishwa katika mafunzo hayo ili wakawe wawakilishi wazuri kwa askari wote wa kike katika Jeshi la Magereza ili kuwajengea uwezo,kukuza uelewa na kuwaunganisha waweze kufanya kazi kw ufanisi zaidi.

“Jukumu mlilopewa na Jeshi la Magereza la uelimshaji ni jukumu muhimu sana katika ustawi wa mtandao wa wanawake ndani ya Jeshi la Magereza, ninahakika,mafunzo mtakayoyapata yatawaongezea uwezo wa kutekeleza jukumu hili muhimu na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya mtando ndani Jeshi,”alisema Bi Mboni

kwa upande wa Mkuu wa dawati la Jinsia Magereza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Bertha Joseph Minde amesema kuanzishwa kwa mtandao wa wanawake magereza kumewawezesha wanawake  Kushika nafasi za juu za uongozi katika Jeshi kama kamishna mmoja,kamshna msaidizi mwandamizi mmoja na makamishn wasaidizi 6 ingawa bado kuna upungufu mkubwa wa kinamama katika nafasi za juu za uongozi.

naye msemaji wa Jeshi la Magereza Mrakibu mwandamizi Amina kavirondo amemuomba Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo Bi  Mboni  kuwashika mkono mtandao wa wanawake Magereza ili kuweza kufikia malengo waliyokusudia

Aidha kamishna msaidizi mwandamizi wa mkoa wa morogoro (RPO)  Ismail T.Mlawa aliwapongeza wanawake wa Jeshi la Magereza kwa kuanzisha mtandao wa wanawake ambapo utawawezesha kupambania haki zao

 mtandao wa wanawake katika Jeshi la magereza ulianzishwa rasmi tarehe7 Desemba,2018 baada ya mkutano wa SADC uliofanyika Dec.2011 nchini Birchhood Johanesburg Africa ya Kusini ambapo katika kikao hicho wazo la mtandao wa wanawake lilirasimishwa na kuwekewa mikakati(the idea of women network consolidation and road map drawn)