Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa kwanza kushoto) akisalimiana na baadhi ya maafisa wa Magereza mkoa wa Morogoro baada ya kuwasili katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Magereza wa mkoa huo leo Julai 27,2018 akiwa katika ziara fupi mkoani humo ikiwa na lengo kuu kuzindua zahanati ya Gereza la Mahabusu.

 

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike amehitimisha ziara yake fupi mkoani Morogoro kwa kuongea na baadhi ya maafisa, askari na watumishi raia wa Ofisi ya Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Morogoro na Gereza Kihonda.

Jenerali Kasike ametumia ziara hiyo ya kwanza tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Jeshi hilo Julai 13 mwaka huu kuwataka watendaji wote ndani ya Jeshi la Magereza kutambua alama za nyakati na kubadilika kabisa kimtazamo, kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kujisikia aibu kwa kuona Jeshi lao linatajwa kwa ubaya wa kushindwa kutimiza majukumu yake sawasawa.

Amewataka maafisa na askari wote kujiandaa kupokea mpango kazi wa kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa ambao hivi sasa unaandaliwa katika ngazi ya makao makuu ya Jeshi hilo.

Jenerali Kasike amewatolea wito viongozi wote ndani ya Jeshi la Magereza kuwa tayari kupokea maoni ya walio chini yao bila kujali vyeo vyao ili kuweza kufikia malengo tarajiwa.

Aidha amesisitiza kuwa ni lazima watendaji wote kufuata maadaili kwakuwa suala la maadili ya kazi halihitaji rasilimali ni mtu kubadilika tu.

(Picha na Jeshi la Magereza)

Kwa habari picha zaidi tembelea www.magereza.blogspot.com