HABARI MPYA Habari zaidi
HISTORIA YA JESHI LA MAGEREZA TANZANIA BARA

1.0.Utangulizi Jeshi la Magereza lilianzishwa rasmi mwezi Agosti 25,1931 baada ya mgawanyo wa majeshi ya Polisi na Magereza kutokea. Licha ya kuwa na majukumu ya kulinda usalama na mali za wageni, kabla ya mwaka 1931 Jeshi la Polisi lilifanya pia kazi za Magereza kama zilivyokuwa kwa tafsiri na madhumuni ya wakoloni. Jeshi la Magereza wakati lilipoanzishwa liliitwa Idara ya Jela ambapo shughuli zake zilibaki kuwa zile za kikoloni za utesaji wa wafungwa pamoja na kazi ngumu bila kujali kama ni ya manufaa kwao au kwa Taifa.

2.0 Dira na dhima ya Jeshi la Magereza

Jeshi la Magereza katika miaka ya 1990 lilianzisha dira na dhima yake kulingana na mabadiliko mbalimbali yaliyojitokeza.Dira ya Jeshi la Magereza ni kuwa Jeshi la kurekebisha wahalifu lenye utaalam wa hali ya juu linaloendeshwa katika kanuni na viwango vilivyowekwa Kitaifa na Kimataifa.

Dhima ya Jeshi la Magereza ni kutekeleza wajibu ipasavyo katika kuimarisha ulinzi wa jamii kupitia usimamizi wa kifungo na kuwasimamia wahalifu, huduma za mahabusu, programu na huduma zinashughulikia mahitaji ya urekebishaji wa wahalifu na ushauri wa Sera kuhusu uzuiaji wa uhalifu na ushughulikiaji wa wahalifu. Soma zaidi>>